Monday 12 May 2014

Kiswahili blog corner: Masuala ya Ngono, Mapenzi na Mahusiano kwa uwazi. Ushauri Karibu tuboreshe, tujifunze na kukumbushana ili sote tufurahie uumbaji wake Mungu.

Siko Comfortable kuwa karibu na Ma'mkwe- Ushauri.
Kiswahili sanifu.

"Hongera sana dada Dinah kwa
jinsi unavyotusaidia kwenye mambo
mbalimbali, nimeshapost maswali
yangu mawili lakini umeyatia
kapuni dada yangu kulikoni??
chonde chonde usilitie na hili
kapuni.
Dinah anasema: Mama M,
sijapokea swali lolote kutoka kwako,
hili ni la kwanza. Kwa kawaida kila
swali linanolifikia ni muhimu na
huwa nali-publish kwa kufuata lini
nimepokea.
*
*

Mimi ni mwanamke niliyeolewa na
nina watoto wawili, mume wangu
alishawahi kunicheat hapo awali
na nikagundua lakini bado
aliendelea. Mpaka sasa bado
sijatulia kutokana na kutendwa na
mume wangu.
Mimi na mama mke hatupatani
kutokana na yeye mama kumtetea
mume wangu alivyonicheat. Mama
huyu alinifokea sana na kuniambia
nimuache mume wangu, Yaani
alinijia juu mpaka wake wa
mashemeji zangu wakawa
wanamsema kwa kumwambia
anavyofanya sio vizuri.
Nimejifungua hivi karibuni na
mtoto sasa anamiezi saba, sijawahi
kuwasiliana na mama mkwe wangu
tangu mwezi wa kumi na mbili
mwaka jana alipokuja kwangu hapa
Dar ambapo aliondoka vibaya na
hata kusema kuwa kamwe hata
kanyaga kwangu.
Mama mkwe yeye anaishi Mkoani,
na kiukweli mimi nilikuwa
nikimuonyesha heshima zote wala
sijawahi kumchukia wala
kujibishana nae sembuse
kubadilishana maneno makali.
Nakumbuka kuna wakati
nilimpelekea nguo za Christmass,
lakini aliziponda sana akasema
atazitupa "nguo gani mbaya
hivyo"? japokuwa ilikuwa ni suti
nzuri tu jamani! mpaka wifi yangu
(mtoto wake) akajisikia vibaya akaja
kuniambia mbele ya mama yake
ambaye aliona aibu na kuanza
kukana.
Tatizo kubwa naona kama huyu
mama mkwe anachuki binafsi na
mimi japokuwa ndio mchezo
wake kwani keshawakorofisha sana
hata hao wake wengine wa
mashemeji zangu ila naona kwangu
kazidi.
Sasa hivi niko kwenye uhusiano
mzuri kiasi na mume wangu japo
bado machungu hayajaisha ila
anajitahidi, aliniita akaniomba
nimsamehe mama yake akidai kuwa
"nyie wanawake mnajuana wenyewe
sijui kwa nini anakuchukia hivyo"
akaniomba nimsamehe na niwe
nampigia simu na niwe karibu nae.
Siku mjibu kitu mume wangu na
wala sikumpigia huyo mama mkwe
kwani mimi nimejifungua hata yeye
angeweza kuja au kunipigia simu
naa kuulizia mtoto lakini anaongea
na mwanae tu.
Swali: Mume wangu anataka
tukambatize mtoto wetu mkoani
(kwa mama mkwe) Xmass hii na
mimi sijisikii huru kwani sitamani
hata kumuona yule mama kwa
alivyonipa stress kwenye maisha
yangu, yani hapa sijaandika yote,
hata watu baki na ndugu zangu
wanajua matatizo niliyoyapata
kutokana na chuki ya mama mkwe.
Naomba ushauri kwanza, nikubali
nikambatizie mtoto huko kwa mama
mkwe au la, na kama nikikubali
kwenda huko je nimnunulie huyu
mama zawadi kama nguo?? kwani
mume wangu huwa hana utaratibu
wa kununua nguo za mama yake
kabisa!! tafadhali nisaidieni nideal
vip na huyu mama??
Wenu mama M"
Dinah anasema: Pole sana
kwa kukabiliana na chuki ya mama
mkwe wako, hili ni tatizo kubwa
linalowakabili wanawake wengi
sana hapa Duniani. Hata mimi
sijui ni kwanini hasa mtu umchukie
mkweo kiasi hicho. Tena mbaya
zaidi ni pale Mumeo akiwa ndio
mtoto wa Kiume kwa kwanza/
mwisho/mtoto wa kiume pekee
kwenye familia yao.....hapa mama
wakwe/wifiz huwa hawataki
mchezo!
Tatizo letu wanadamu huwa
tunategemea kupendwa mara tu
baada ya kuungana na familia
nyingine (kufunga ndoa), Jamani!
Mtu mmoja kukupenda haina
maana Ukoo mzima ukupende.
Kama ikitokea kwa bahati nzuri
mkapendana poa, ikitokea
hawakupendi safii tu au kama
wewe huwapendi ni kawaida
vilevile (kwani mlizaliwa pamoja
bwanaaa!).....kitu muhimu ni
kuheshimiana na kila mmoja wenu
kujua mipaka yake kati ya yule aliye
waunganisha in ur case mumeo.
Unachotakiwa kuzingatia ni Kumpa
heshima lakini kamwe
usijipendekeze kwa mama mkwe
huyo, usijilazimishe kumpenda
(huwezi kulazimisha hisia kama
hazipo kubali kuwa hazipo),
kutokumchukia (mchukulie kama
alivyo na dharau uchokozi na chuki
zake kwako), hata siku moja
usimzungumzie vibaya kwa watu
wengine (kwa kufanya hivyo
itakufanya ujenge chuki dhidi yake)
kumbuka kuwa huyo ni bibi wa
watoto wako hivyo kubali kuwa
hakupendi na muache kama alivyo
aili mradi tu hamkai nyumba moja.
Ni kama kuwa Kazini/Shuleni,
kutakuwa na watu wanakupenda na
wengine hawakupendi(ni nature ya
mwanadamu)....... lakini huwezi
kuacha kazi au masomo kwa vile tu
watu fulani wanakuchukia.
Unawadharau na kufanya kazi/
masomo yako kwa bidii.
Ukiangalia kwa undani asilimia
kubwa ya wanawake huwa na tabia
ya kuchukiana kweli kweli bila
sababu, inawezekana kabisa mtu
humjui lakini unajenga chuki. Sasa
mimi nadhani hii asili ya baadhi ya
wanawake kuwa na chuki za ovyo-
ovyo ndio husababisha baadhi ya
wakwe zetu kuwa hiyo kwani
uanamke hauwatoki hata kama ni
watu wazima sana.
Wataalam wa Saikolojia wanadai
kuwa mama na mtoto wa kiume
huwa na bond maalum, ukaribu
huo kati ya mama na kijana wake
kuendelea kwa muda mrefu sana.
Mama huyu huendelea kudhani
kuwa Kijana anahitaji kumsikiliza
na kufanya maamuzi ambayo yeye
mama anakubaliana nayo kama
akipinga basi Kijana hapaswi
kuendelea na maamuzi hayo na
kiendelea basi atakumbwa na
mabaya (si umewhai kusikia kuwa
Radhi ya mama ni Kali kwa mtoto
wa kiume kuliko wa kike? Jiulize
kwanini iwe kwa mtoto wa kiume
tu?).
Sasa Kijana anapokuwa na kuanza
kujitegemea mama hupata hisia za
kupoteza sehemu kubwa maisha
yake na hivyo ataendelea kujiweka
karibu na kutaka kujua kila kitu
ambacho Kijana wake anakifanya.
Ikitokea Kijana kaamua kuchumbia
Binti ampendae mama huyu
anaweza kukubali au kupinga
(huwezi kuambiwa hili ni suala la
familia yao).
Mama akikubali basi ataanza
kujiweka sana kwenye uhusiano
wenu na kuhoji vitu kama vile
mtafunga ndoa lini? nani
asimamie, aina ya nguo zitakazo
valiwa, sherehe iwe wapi na iwe
vipi? n.k. Baada ya kufanikiwa
kufunga ndoa mama huyu ataanza
"nataka mjukuu" wakati tayari wapo
wengine waliozaliwa na dada/kaka
wa mumeo....
Hii yote ni katika kutafuta ushindi
na kukuonyesha wewe Mkwe
(anakuona kama mwanamke
mwingine unaechukua nafasi yake
kwa mwanae) kuwa yeye ndio
mwenye sauti na mamlaka kwani
huyo Mumeo ni mtoto wake hivyo
anatakiwa kufanya akisemacho yeye
na sio wewe.
Kutokana na maelezo yako
inaonyesha kuwa Mama mkwe wako
hakupewa nafasi sana kwenye
uhusiano wenu na ndio maana
anakuwa bitter kila kukicha, na
kilichonifanya nigundue hilo ni
kutokana na maelezo yako kuwa
alimtetea mwanae alipotoka nje ya
ndoa.....alimtetea mwanae ili
aweze kum-win back Kijana wake
na wewe ubaki mwenyewe na
maumivu yako moyoni.....alitaka
Ushindi kwani wewe ndio
unaemjali kwa kumnunulia zawadi
na si mwanae......kwa mama mkwe
huyu hili ni pigo kubwa kwani
anadhani kuwa wewe as
"mwanamke tu" ndio una-control
kila kitu kwenye maisha ya
mwanae.
Nini cha kufanya: Mimi binafsi
sioni sababu yakwenda kumbatiza
mtoto huko Mkoani unless
otherwise kuna sababu za msingi
kama vile Kabila la Wachaga (Xmas
kuliwa Nyumbani Moshi kind
muhimu), mnamtegemea yeye
Mama mkwe kiuchumi, labda ndugu
wengi wako huko Mkoani na
wanataka kushuhudia Ubatizo na ili
ku-save ni bora ninyi muende huko
kuliko wao kuja Dar, Mama mkwe
huyo mgonjwa na hawezi kusafiri
lakini anataka kumuona mtoto n.k.
Ili kuondoa vurugu, wewe kubali
kwenda kubatiza mtoto huko aliko
mama mkwe lakini hakikisha
unaelewana na mumeo kuwa
hamkai sana ili kuepuka
"chokochoko" za huyo mwanamama.
Utakapo kwenda huna haja ya
kumnunulia chochote huyo
mwanamama asie na shukrani.....ili
apate ujumbe kuwa kuponda
zawadi =hakuna zawadi.
Baada ya shughuli ya Ubatizo
kuisha ni vema wewe na mumeo
kuwasiliana kwa mara nyingine
tena kuhusiana na unavyojisikia
kwa mama mkwe wako.
Usipozungumza na mumeo na
kuliweka hili wazi na kumfanya
akuelewe ili asaidie kumaliza chuki
za mama yake kwako.
Mumeo mpenzi ataendelea kudhani
(mwanaume akisema "sijui kwanini
mnachukiana, ni mambo yenu
wanawake...naomba umsamehe
mama") yaya tachukulia kuwa
yameisha, kuwa umemsamehe
mama yake na hivyo kuendelea
kufanya mambo ya kumhusisha
mama yake na wewe mara kwa
mara hali itakayosababisha
maumivu makali ya hisia kwa vile
utadhani kuw amumeo hakujali pia
hautokuwa comfortable na mkweo.
Liweke wazi suala la wewe kujisikia
huna thamani kwa mama mkwe
huyo kutokana na dharau zake,
kutetea usaliti wa ndoa...tena
sisitiza hapa kuwa ukimuona mama
mkwe huyo unakumbuka uchafu
aliokufanyia mumeo (umesema
kuwa bado unamachungu/
hujasahau japokuwa unajitahidi
kusamehe....itachukua muda
mpaka kurudia hali yako ya
kawaida). Mwambie yote yalioujaza
moyo wako bila hasira wala chuki.
Muombe mumeo amwambie na
ikiwezekana amsaidie mama yake
abadilishe tabia yake mbaya, na
mara baada ya kubadilisha tabia
yake basi anza kumnunulia/tumia
zawadi lakini sio ktk kujipendekeza
bali kumjali.
Nani alisema maisha ya ndoa ni
rahisi eei? Ni magumu ila ukijua
namna ya kukabiliana na wanawake
(mama mkwe/wifi) kila kitu kina
kinaenda vema na kila mmoja
wenu anafurahia maisha yake
kivyake na familia yake.
Natumaini kuwa maelezo ya
wachangiaji na haya yangu
yatakuwa yamekusaidia kufanya
uamuzi wa busara.
Kila la kheri!

Kiswahili kitukuzwe , chuo Kikuu, vyuo vikuu

0 comments:

TRENDING THIS WEEK

SPORTS